TANGAZA NASISI

TANGAZA NASISI
bei zetu ni nafuu sanaaaaa

matangazo


Friday, November 13, 2015

CHUO CHA MAISHA

        CHUO CHA MAISHA

Wasalesiani wa Don Bosco kupitia kitengo cha miito kwa vijana wanaendesha program ya chuo cha maisha maparokiani .Mwaka jana tulikuwa na parokia nne ambazo ni Mwenge, Magomeni, Msimbazi na Kibaha. Jumla ya vijana waliohitimu ni 160. Program hii ipo chini ya Padri Augustine Sellam pamoja na timu nzima ya Y4Y ambao ni wakufunzi Alex, Augustine, Calistus, Cassian, Erick, Frank, Flora, Faustino, Gloria, Gilbert, Jack, Joseph, Joyce, Neema, Modest, Oliver, Prosper,Sarah na Hyacinta pia tunapokea wanachama wapya ambao wamehitimu mafunzo ya chuo cha maisha ili kuendelea kuwasaidia vijana wengine
MALENGO YA CHUO CHA MAISHA
Kuwasaidia vijana kujua stadi za maisha ya kikristu kuendelea kukua katika maadili .Mafanikio ya chuo cha maisha ni makubwa kwa vijana tumekutana na vijana wengi wanasema inawasaidia kujitambua kama vijana wakatoliki kujua umuhimu wao katika kanisa Wanasema mada ni nzuri kwa sababau zinagusa sehemu zote, Kiroho, Kimwili, Kijamii na Kiakili. Pia Maparoko na walezi wa vijana wanaipongeza program hii kwamba inawasaidia vijana wao kutambua wajibu wao wanaomba program hii iwe inawafikia vijana wao mara kwa mara. Kulingana na mahitaji ya vijana Don Bosco Youth Ministry imeandaa program ya Chuo Cha Maisha kwa Dar es Salaam mwaka huu parokia tano ambazo ni parokia ya Tabata, Kawe, Mbezi Beach, Tageta na Yombo Dovya inawafikia na  kuwasindikiza vijana miezi kumi. Vijana hushiriki mafungo ya kiroho pamoja na timu nzima ya Y4Y ambao wanakutana jumaosi ya kwanza ya mwezi kwa ajili ya tathimini.
MAFUNGO
pia huwaga kunakua na mafungo baada ya kupata elimu ya chuo chamaisha nikira mwaka mwezi wa kumina mbili.
FAIDA YA MAFUNGO
1.kujijenga upya kiroho  na kimwili.
2.jenga afya kupitia utulivu ulio huko katika maisha
3.kupata malafiki tofauti tofauti na kujuana na watu wengi
ENEO
mafungo haya huwa yanafanyika MBAGARA spiritual centre au tembelea DONBOSCO upanga kwa maelezo zaidi
Mr. Alexander
Don Bosco Upanga

No comments:

Post a Comment